Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (2024)

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo kuhusu taarifa
  • Author, Kateryna Khinkulova
  • Nafasi, BBC World Service

Uvamizi wa Ukraine katika eneo la Urusi tarehe 6 Agosti ulipokelewa kwa mshangao sio Moscow pekee, bali pia kwa raia wa Ukraine hasa wale wanaofuatilia vita hivyo kutoka nje ya nchi.

Kwa nini Kyiv iliamua kufanya shambulio hili la kushtukiza? Hili ni swali ambalo watu wanajiuliza hasa ikizingatiwa kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kuingia karibu kilomita1,000 ndani ya Urusi na takriban wiki moja baadaye, jeshi la Urusi bado linajitahidi kuzuia uvamizi huo. Lengo la operesheni hiyo inaanza kuibuka.

Haya hapa ni maswali matano muhimu kuhusu matukio mapya katika vita vya Ukraine ambayo huenda yakachagiza jinsi mambo yatakavyoendelea katika miezi ijayo.

Nini kilifanyika mjini Kursk?

Tarehe 6 Agosti vikosi vya Ukraine vilifanya mashambulizi ya kushtukiza katika eneo la Kursk nchini Urisi, linalopakana na Ukraine. Hakuna haarifa za kuaminika kuhusu ukubwa wa shambulio hilo zimekuwa haba.

Hapo awali, ilionekana kuwa operesheni hiyo ilikuwa katika kiwango cha uvamizi wa mara kwa mara wa vikundi vya hujuma vya Urusi, kinyume na serikali ya Vladimir Putin. Walikuwa wamejaribu kuja Urusi kutoka Ukrainia na walionekana kuhusisha mamia ya wafanyakazi wa kabila la Kirusi.

Lakini shambulizi hili la hivi punde liliposonga zaidi katika eneo la Urusi - huku wanablogu wa kijeshi wa Urusi wakiripoti mapigano makali umbali wa kilomita 30 kutoka mpakani na gavana wa eneo la Kursk akimwambia Rais Putin kwamba vijiji 28 vya Urusi viko mikononi mwa Ukraine, ikawa wazi kuwa wanajeshi wa kawaida wa Ukraine walihusika.

Soma pia:
  • Kwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?

  • Urusi yaongeza mashambulizi dhidi ya wakosoaji wake nje ya nchi

Inaonekana wakati Urusi ilikuwa inaelekeza nguvu zake za kijeshi katika maeneo kadhaa muhimu ya mstari wa mbele ambapo mapigano yanaendelea kuwa mazito, Ukraine iliamua kuchukua fursa ya mpaka huo uliokuwa na ulinzi mdogo na kuvuka hadi ndani ya Urusi.

Afisa mkuu wa usalama wa Ukraine ambaye jina lake halikutajwa ameliambia shirika la habari la AFP: "Tuko kwenye mashambulizi. Lengo ni kumvuruga adui, kumtia hasara kubwa na kuyumbisha hali ya Urusi kwani hawawezi kulinda mpaka wao wenyewe.

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (3)

Kwa nini Ukraine ilishambulia Urusi katika eneo la Kursk?

Mwanzoni Kyiv ilikaa kimya kuhusu shambulio hilo, lakini rais Volodymyr Zelensky alithibitisha uvamizi huo kwa njia isiyo ya moja kwa moja tarehe 10 Agosti.

Alidai kwamba Ukraine iliendelea "kuelekeza vita kwenye eneo la wavamizi". Hakutoa sababu za wazi au malengo ya operesheni hiyo, lakini mnamo Agosti 12 alitangaza kuwa karibu kilomita 1,000 mraba za eneo la Urusi sasa zilikuwa chini ya udhibiti wa Kyiv.

Wachambuzi wa kijeshi na kisiasa wanaojaribu kujibu swali la "kwa nini", wanakubali zaidi kwamba kuvuruga kwa mbinu kunaweza kuwa mojawapo ya malengo makuu ya uvamizi huu.

Kwa miezi kadhaa iliyopita, Ukraine ilijitahidi kuzuia vikosi vya Urusi mashariki mwa Ukraine, ambavyo vimekuwa vikisonga mbele, na kuuteka mji wa kimkakati wa Chasiv Yar mwezi uliopita. Katika maeneo ya kaskazini-mashariki na kusini, hali ni ngumu pia.

Licha ya kuzidiwa nguvu na Urusi katika maeneo mengi ya mstari wa mbele wa kilomita 1,100, mamlaka ya Ukraine iliamua kucheza kamari ili kuunda eneo la mapigano lililo umbali wa mamia ya maili, ili kumfanya mpinzani kutumia rasilimali zake, na kuelekeza shinikizo kutoka mashariki mwa Ukraine. eneo la Kursk nchini Urusi.

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Reuters

Mtaalamu wa masuala ya usalama profesa Mark Galeotti aliiambia BBC kwamba Ukraine imenaswa katika vita vya uhasama kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita, huku kukiwa na harakati kidogo ardhini, sasa inahitajika kupata faida ya hatua yake ya sasa.

Manauchumi huyo, pia alisema hii ilikuwa kamari: "Tulituma vikosi vyetu vilivyokuwa tayari kwa mapigano kwenye sehemu dhaifu zaidi ya mpaka wao". Aliongeza kuwa hatua hiyo imefikia haraka lengo la Kyiv kuliko ilivyotarajia.

"Makamanda wao sio wajinga ... wanaleta vikosi vyao mbele, lakini sio haraka kama tunavyotaka. Wanajua hatuwezi kutanua wigo wetu zaidi ya kilomita 80 au 100.

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (5)

Chanzo cha picha, AFP

Urusi imeitikiaje?

Vyombo vya propaganda za Urusi ziliandika haraka juhudi za kudhibiti uvamizi wa Ukraine na kuziita "operesheni ya kupambana na ugaidi".

Hadi watu 121,000 wameambiwa kuhama kutoka eneo la Kursk na wengine 11,000 walihamishwa kutoka eneo jirani la Belgorod. Mamlaka ya Urusi ilitangaza hali ya dharura katika eneo hilo na kutoa fidia ya $ 115 kwa wakazi wa eneo hilo.

Mkuu wa Jeshi la Urusi, Jenerali Valery Gerasimov alidai mara kadhaa wiki iliyopita kwamba uvamizi wa Ukraine umesimamishwa, kiuhalisia mambo yalikuwa tofauti.

Jenerali Gerasimov hakuwa katika mkutano wa hivi punde zaidi wa Baraza la Usalama la Urusi, chini ya uenyekiti wa Rais Putin, uliojitolea kusuluhisha mzozo huu. Kwa upande mwingine, mashirika wa karibu wa Putin alikuwepo, mkuu wa huduma ya usalama ya Urusi FSB, Alexander Bortnikov.

Katika taarifa yake ya hivi punde kuhusu matukio hayo, Rais Putin ameishutumu Ukraine kwa kushambulia raia wake na kuahidi "jibu linalostahili".

Profesa Galeotti anasema Ukraine inakabiliwa na hatari ya Urusi kulipiza kisasi kutoka.

"Putin anaweza kuanzisha wimbi lingine la uhamasishaji na kujumuisha askari laki kadhaa kwenye vikosi vyake vya jeshi."

Anaongeza kuwa Urusi inaweza kutafuta njia zingine za kuzidisha mzozo huo. Katika miezi ya hivi karibuni Ukraine imekabiliwa na mashambulizi ya mabomu ya Urusi yaliyolenga miundombinu yake ya nishati. Mapambano yatakayofuata uvamizi huu wa Ukraine yatakuwa makali zaidi.

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (6)

Je, mapigano ya Kursk yanamaanisha Ukraine iligeuza mkondo wa vita?

Hatua ya Ukraine kuvamia Urusi inahitaji ikiwekwa kwenye mizani- huenda taifa hilo lisishangilie mwisho wa mzozo huu hivi karibuni.

Kama anavyosema Mark Galeotti, "ni eneo la takriban maili 50, katika muktadha wa ukubwa wa Urusi na Ukraine, hilo haliwezekani. Lakini athari za kisiasa ni muhimu zaidi.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa Ukraine ilikuwa na nia ya kuonyesha washirika wake wa Magharibi, hususan Marekani hasa, kwamba majeshi yake yana uwezo wa kuendelea na mapigano. Hii pia imeimarisha, angalau kwa muda, nguvu ya mazungumzo ya Kyiv: na askari wao waliopo kilomita 30 ndani ya eneo la Urusi.

Operesheni hiyo pia imebadilisha mtazamo wa vita hivi na kwa Warusi ndani ya nchi - huu sio tena mzozo wa mbali unaoitwa "operesheni maalum ya kijeshi", bali ni mzozo unaowaathiri moja kwa moja.

Mwandishi wa BBC wa Ulaya Mashariki Sara Rainsford anasema: "Ukifuatilia kwa makini baadhi ya ripoti zinazotoka eneo la Kursk, hata kwa kuzingatia mazingira yaliyodhibitiwa ya vyombo vya habari vya Urusi, ni wazi kwamba baadhi yanauliza maswali."

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (7)

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Je, uvamizi huu utaathiri vipi mustakabali wa Zelensky na Putin?

Kwa viongozi wa Urusi na Ukraine huu ni wakati mahimu wa urais wao.

Kwa Vladimir Putin, kiongozi wa kiimla wa muda mrefu asiyebadilika, ambaye amezoea kutegemea wandani wake hususanwa huduma wa usalama, uvamizi huu unaleta changamoto kubwa. Ni vigumu kubaini kiwango cha majeruhi wa jeshi la Urusi. Kutokana na idadi kubwa ya Warusi (maelfu) na kwamba hatua hiyo haijafikia vita kamili.

Kama anavyosema Mark Galeotti, "kila wakati Kremlin inazidi kuimarisha propaganda."

"Tumeona hili katika vita vya zamani, kutokazama za vita vya Usovieti huko Afghanistan hadi vita vya Urusi huko Chechnya, Kremlin inaweza kudumisha msimamo fulani lakini baada ya muda, ukweli unabainika."

Kwa Volodymyr Zelensky uvamizi nchini Urusi unaweza kugeuka kuwa ngumu sawa, lakini kwa sababu tofauti.

Mchanganuzi Emil Kastehelmi anasema matokeo bora zaidi kwa Ukraine ni kwamba Urusi inaelekeza "rasilimali nyingi kutoka sehemu muhimu zaidi ili kukomboa [eneo la Urusi] lililotekwa."

Kuongeza matumaini ya watu wa Ukraine kwa muda mfupi, kunaweza kusababisha hasara kubwa zaidi katika eneo la mashariki, ambapo mapigano yanaendelea kuwa mazito na baadhi ya wanablogu wa kijeshi wa Urusi wanasifia hatua iliyopigwa, ingawa madai yao hayajathibitishwa kwa sasa.

Profesa Galeotti anasema msukosuko wa sasa katika vita ulihitaji ili kubadili mkondo wa mambo. Matokeo ya mabadiliko hayo hayajakuwa wazi.

Maelezo zaidi:
  • Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwa

  • Je vita vya Urusi nchini Ukraine vinakwenda kama Urusi inavyotaka?

  • Ukraine inaweza kushindwa vita 2024. Hivi ndivyo inavyoweza kutokea.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Rueben Jacobs

Last Updated:

Views: 5694

Rating: 4.7 / 5 (57 voted)

Reviews: 80% of readers found this page helpful

Author information

Name: Rueben Jacobs

Birthday: 1999-03-14

Address: 951 Caterina Walk, Schambergerside, CA 67667-0896

Phone: +6881806848632

Job: Internal Education Planner

Hobby: Candle making, Cabaret, Poi, Gambling, Rock climbing, Wood carving, Computer programming

Introduction: My name is Rueben Jacobs, I am a cooperative, beautiful, kind, comfortable, glamorous, open, magnificent person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.